Neymar kufanyiwa upasuaji
MSHAMBULIAJI wa Brazil, Neymar Santos amedokeza jeraha alilopata juzi dhidi ya Uruguay kuwa linahitaji upasuaji.
Neymar alitolewa katika mchezo huo baada ya kuumia kifundo cha mguu hata hivyo Brazil ilipoteza mabao 2-0.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Neymar amesema: “Sio rahisi kupata majeraha na kufanya upasuaji na unafanya hivyo ikiwa miezi minne tu baadaye.”
Neymar amesema kwa sasa anahitaji sapoti ya familia yake na marafiki pengine muhimu zaidi kuliko ilivyowahi kuwa kwenye nyakati zingine.