Neymar kuikosa Bayern

NYOTA wa PSG, Neymar atakosa mechi ya raundi ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern Munich kutokana na jeraha la kifundo cha mguu, kocha wa timu hiyo, Christophe Galtier amesema.

Mshambuliaji huyo wa Brazil alitolewa nje akiwa na jeraha la kifundo cha mguu wa kulia wakati PSG iliposhinda 4-3 nyumbani dhidi ya Lille Februari 19.

“Hatutakuwa na Neymar kwa michezo miwili ijayo,” Galtier alisema jana, na kudai kuwa ni “hasara kubwa,” “Badala ya kuwa na viungo wawili, tutakuwa na viungo watatu na washambuliaji wawili.”aliongeza

Kylian Mbappe na Lionel Messi huenda wakaunda safu ya mbele ya PSG kwa mechi ya mkondo wa pili Jumatano.

Vinara hao wa Ligue 1 wako nyuma kwa bao 1-0 lililofungwa na Kingsley Coman katika mchezo wa raundi wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Parc des Princes 14 Februari.

PSG pia itawakosa kiungo Renato Sanches na mlinzi Presnel Kimpembe kutokana na majeraha watakapowakaribisha Nantes kwenye mechi ya ligi kuu ya Ufaransa leo.

Habari Zifananazo

Back to top button