Neymar Kuikosa Copa America 2024

BRAZIL: DAKTARI wa timu ya taifa ya Brazil, Rodrigo Lasmar amesema nyota wa taifa hilo, Neymar Jr atayakosa Mashindano ya 48 ya Copa América mwakani.
Dk Lasmar kupitia vyombo vya Habari vya Kimataifa ameeleza ni ngumu kwa, Neymar (31) kushiriki michuano hiyo itakayotimua vumbi Juni 20-Julai 14, 2024 nchini Marekani.
 
“Hakutakuwa na muda wa ziada kusubiri, hakuna uwezekano kwa Neymar kupona majeraha yake ya goti mapema” amesema Daktari huyo.
 
Amesema, hawapo tayari kutumia njia za mkato kumuwezesha mfungaji bora wa muda wote wa Brazil kurejea uwanjani mapema.
 
“Matarajio ni kwamba atakuwa tayari kurejea mwanzoni mwa Agosti, 2024.” Amesema Dk Lasmar.
 
Mchezaji huyo wa Al Hilal ya Saudi Arabia alipata majeraha mwezi Oktoba, 2023 katika mchezo dhidi ya Uruguay kuwania kufuzu Michuano ya Kombe la Dunia.
Mashindano ya Copa America mwakani yatafanyika nchini Marekani ikiwa na makubaliano ya vyama vya mpira wa miguu barani America Kusini na America Kaskazini.

Habari Zifananazo

Back to top button