Ngorongoro kuwania Tuzo Kivutio Bora

ARUSHA; Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), imeteuliwa kuwania Tuzo ya Kivutio Bora cha Utalii Duniani mwaka 2024.

Kaimu Kamishina wa Uhifadhi NCAA, Victoria Shayo amesema dirisha la kupiga kura limefunguliwa leo Aprili 28, 2024 na kutoa rai kwa wadau wa utalii kupigia kura hifadhi hiyo, ili iweze kushinda kutokana na aina ya vivutio vilivyopo.

“Kura yako ni ushindi wetu  licha ya eneo kuwa kivutio bora cha Utalii, lakini pia eneo hilo linasifika kuwa na hadhi ya kipekee Kusini mwa Jangwa la Sahara  kutokana na aina ya vivutio vya utalii vilivyopo, ” amesema.

Amesema nchi tano zinawania tuzo hizo ambazo ni Afrika Kusini, Misri, Botswana, Malawi na Tanzania hivyo ni wakati sasa wa wadau kupiga kura, ili NCAA iweze kushinda tena tuzo hiyo.

“NCAA ikishinda itawezesha hifadhi kukua kiuchumi zaidi sanjari na watalii wengi kutembelea hifadhi, hivyo tunawaomba mpigie kura kupita https://www.worldtravelawards.com/vote-r3#votenow ili tushinde” amesema.

Naye Peter Makutian ambaye ni Ofisa Utalii Mkuu,  amesema upigaji kura huo ni muhimu kwa ajili ya kuwezesha mamlaka hiyo kupata ushindi wa tuzo hiyo.

Habari Zifananazo

Back to top button