Ngrongoro wajipanga matumizi ya ardhi

Ngrongoro wajipanga matumizi ya ardhi

MKUU wa Wilaya ya Ngorongoro, Raymond Mwangwala, amesema kuwa Halmshauri ya Wilaya ya Ngorongoro, kwakushirikiana na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi,  imeanza uandaaji wa mpango wa matumizi ya ardhi utakaodumu kwa zaidi ya miaka 20

Mpango  huo wa matumizi ya ardhi wa halmashauri hiyo, utatoa taswira sahihi ya matumizi ya ardhi, ikiwemo malisho, kufanya ufuatiliaji wa mabadiliko ya matumizi  ya ardhi na kubaini athari zake kiuchumi pamoja na mabadaliko ya tabianchi.

Dc Mangwallah alitoa rai hiyo leo  wilayani Ngorongoro, wakati akifungua kikao cha uandaaji wa mpango wa matumizi ya ardhi wa halmashauri ya wilaya hiyo na kusisitiza wadau walioshiriki mkutano huo kutoa maoni yao, ili ardhi hiyo iweze kupangwa vema.

Advertisement

Amesema  mpango huo utasaidia watumiaji mbalimbali  wa ardhi, kutambua ukubwa,ikiwemo vijiji kujikwamua kiuchumi kwa kuanisha maeneo muhimu kwa ajili ya uchumi kukua.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Jumaa Mhina amesema awali vijiji 36 vilipimwa na serikali, huku mpango huo utawezesha vijiji kujulikana kisheria sanjari na kupanga matumizi sahihi ya maeneo mbalimbali ya kilimo,mifugo, utalii na sekta nyingine muhimu za kuinua uchumi, ikiwemo upatikanaji wa hati za kimila na kuondoa migogoro.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Soitsambu , Marko Lorasha ameipongeza serikali kwa kusimamia mpango huo kikamilifu, kwani utawasadia kuondoa migogoro ya ardhi iliyokuwepo awali wilayani hapo sanjari na vijiji kunufaika na ardhi yao.