Ngumi Temeke kumpa tuzo Rais Samia

CHAMA cha ngumi za ridhaa wilaya ya Temeke kwa kushirikiana na kampuni ya Gogopowa Sports & Entainment, wameaandaa tuzo maalumu ya Rais Samia Suluhu Hassan itakayofanyika Oktoba 30 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Tuzo hiyo itaambatana na bonanza la ngumi ambalo litahusisha mapambano ya mabondia wa zamani na vijana katika kuhamasisha mchezo huo. Mratibu wa tuzo hiyo Said Omary ‘Gogopowa’, alisema Dar es Salaam jana kuwa lengo ni kutambua mchango wa Rais katika kuwekeza kwenye michezo nchini.

Alisema kuwa maandalizi yanaendelea kufanyika kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Wilaya Temeke ili jambo hilo lifanyike kwa weledi.

“Sisi wanamasumbwi tumeona tutoe tuzo ya heshima kwa Rais ambaye amekua mstari wa mbele katika kuwekeza kwenye michezo hususani ngumi ambayo inapiga hatua kubwa kadri miaka inavyosogea,” alisema Gogopowa.

Alitoa wito kwa wadau kujitokeza kwa wingi kusaidia na kuunga mkono ili kufanikisha tukio hilo.​​​​​​​

Habari Zifananazo

Back to top button