Ngushi kukipiga kwa Wagosi wa Kaya

MSHAMBULIAJI wa Yanga Chrispin Ngushi rasmi sasa atakipiga Coastal Union kwa mkopo hadi mwishoni wa msimu.

Ngushi alisajiliwa Yanga akitokea Mbeya Kwanza misimu miwili iliyopita ambapo alikosa nafasi ya kucheza na kushuka kiwango chake.

Ngushi ambaye alipewa nafasi ya kuonesha makali ndani ya kikosi kilichoshiriki Michuano ya Kombe la Mapinduzi, ameshindwa kulishawishi benchi la ufundi la klabu hiyo na kuondolewa kwenye mipango ya timu msimu wakati dirisha dogo la usajili likiwa linaendelea.

Wakati anasajiliwa na Yanga dirisha dogo la usajili msimu wa 2021/2022, ilielezwa kwamba Kigogo mmoja klabuni hapo alisafiri kwa ndege hadi Jijini Mbeya kunasa saini ya winga huyo aliyeng’ara wakati ule akiwa na Mbeya Kwanza FC.

Timu alizopitia ni, Kyela Combine (Mbeya ), Boma Fc (Mbeya), Mbeya Kwanza Fc, Yanga Sports Club na hivi sasa Coastal Union.

Habari Zifananazo

Back to top button