Nguvu kazi ujenzi wa madarasa wamshawishi Dk Kiruswa

NGUVU kazi ya Wananchi wa kata ya Gelai Meirugoi wilayani Longido mkoani Arusha juu ya ujenzi wa madarasa sambamba na kuchangishana Sh milioni 16, imemshawishi Naibu Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo hilo, Dk Steven Kiruswa kuunga mkono juhudi hizo.

Dk Kiruswa ameahidi kutoa maji katika vyanzo vya maji umbali wa Km 10 hadi katika eneo la ujenzi wa madarasa hayo na kumalizia ujenzi wa choo cha walimu kwa gharama ya zaidi ya Sh milioni 4.

Akizungumza katika kitongoji cha Ngoingoi kijiji cha Melolugoi katika kata hiyo baada ya kushiriki nguvu kazi ya ujenzi wa madarasa mawili na ofisi ya walimu ,Dk Kiruswa alisema jitihada hizo zinapaswa kuungwa mkono na marafiki zake wa Marekani wenye Shirika lisilo la Kiserikali la Friends For African Development (FAD).

Kiruswa akishiriki nguvu kazi ujenzi wa madarasa kitongoji cha Ngoingoi

Alisema awali alitoa Sh milioni 8 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili na nyumba ya walimu na Wananchi wamejichangisha zaidi ya Sh milioni 16 jitihada hizo zinapaswa kupongezwa kwa dhati na kuungwa mkono.

Waziri Kiruswa alisema serikali ya Rais Samia Suluhu Hasssan haitawaacha katika kuchangia jambo hilo kwani Rais anawajali Wananchi wake hususani wa jimbo la Longido na vitongoji vyake kwa kutoa fedha za umaliziaji madarasa na hata ujenzi wa madarasa mengine ili shule hiyo iweze kusajiliwa rasmi.

‘’Nimeguswa na mwamko huu wa wananchi wa kujitoa kwa nguvu kazi na kuchangishana hata yeye imemgusa na kuona sasa jamii ya kifugaji imeamka na kuhitaji elimu kwa Watoto wao.

’’alisema Kiruswa.

Kiruswa na nguvu kazi ujenzi wa madarasa kitongoji cha Ngoingoi Longido

Awali diwani wa kata hiyo, mchungaji Daniel Nasinda alimweleza Dk Kiruswa kuwa changamoto kubwa inayowakabili katika ujenzi wa madarasa hayo ni ubovu wa barabara kwani wenye magari ya usafiri wamekuwa wakigoma kusafirisha vifaa vya ujenzi madai kuwa barabara inayokwenda katika eneo hilo ni mbaya na inauwa magari yao.

Nasinda alisema na kumuomba mbunge kuwasiliana na Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) wilayani Longido ili kuitengeneza barabara hiyo ili shughuli za ujenzi wa madarasa ziweze kwenda kwa kasi kuliko ilivyo sasa kwani inafanyika kwa kusuasua pamoja na wananchi kujitoa.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Londolwa, Lepilal Kiambwa Mollel pamoja na kuwashukuru FAD kwa uanzishwaji wa darasa moja lililojengwa na Wamarekani hao na kuzaa madarasa mengine 11 changamoto nyingine ni uhaba wa madawati kwani madarasa yanaongezeka na mahitaji madawati yanahitaji hivyo alimuomba mbunge na FAD kuwasaidia.

Habari Zifananazo

Back to top button