NHIF wakanusha kumkataa Mkurugenzi Mkuu

WAFANYAKAZi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wamepinga taarifa kuwa hawamtaki Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Bernard Konga.

Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) tawi la NHIF kimesema kimesema taarifa zilizochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa Jamii Forums si za kweli.

Tamko la TUGHE lilieleza kuwa Agosti 19 mwaka huu mtandao huo ulichapisha habari yenye kichwa ‘Watumishi wa NHIF hatumtaki Mkurugenzi Mkuu, Bernard Konga kutokana na uongozi mbovu, uliojaa upendeleo na uonevu’.

“Pia tarehe 24/08/2022 ilichapishwa habari nyingine yenye kichwa cha habari ‘Mkurugenzi Mkuu anakivuruga Chama cha Wafanyakazi (TUGHE)’ lilieleza tamko hilo lililosainiwa na Mwenyekiyi wa tawi, Edwin Chitage na Kaimu Katibu wa tawi, Dk Gwamaka Edward.

TUGHE NHIF kimeeleza kuwa matamko hayo si msimamo wa chama cha wafanyakazi na pia si msimamo wa watumishi wa NHIF.

Tamko hilo lilieleza kuwa chama cha wafanyakazi kimekuwa mstari wa mbele kudumisha kuna utulivu na uhusiano bora mahala pa kazi.

“Kwa tamko hili chama cha wafanyakazi kinalaani wote waliotoa taarifa hizo za uzushi na tunatoa wito kwa jamii kupuuza taarifa hizo. Sambamba na hili tunaomba mamlaka husika zichukue hatua stahiki dhidi ya wahusika” lilieleza tamko hilo.

Agosti 09, 2017 Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, Dk John Magufuli alimteua Konga kuwa Mkurugenzi Mkuu NHIF. Kabla ya uteuzi huo Konga alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button