TANGA: MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga umebaini uwepo wa wanachama hewa wasio halali zaidi 130 waliopata huduma kwenye vituo vya kutolea huduma wakati walipoendeza zoezi la uhakika wa huduma zao
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Tanga Evans Nyangasa wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya biashara na utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Usagara Jijini humo.
Amesema uhakiki huo ulifanyika kati ya mwezi June 2023 mpaka sasa na katika udanganyifu huo kuna baadhi ya waliotumia huduma hizo wamezilipia gharama ambazo walitumia ndivyo sivyo huku wakitoa wito kwa watoa huduma kutoa kwa mwanachama sahihi na kwa wakati sahihi na huduma halali.
“Tumejipanga kutoa huduma kwa wananchi kwenye nyumba za ibada,mashule na vijiji ili waweze kujiunga na bima ya afya lengo lao ni kuhakikisha kila mwananchi anajiunga na mfuko huu”alisema.