Ni uwekezaji mkubwa Afrika

MKONGO wa Mawasiliano wa Baharini (Submarine Cable) wa 2 Afrika na Teknolojia ya Mawasiliano ya kasi ya 5G ya Airtel unaunganisha nchi 35 barani Afrika na mabara matatu ambayo ni Afrika, Asia na Ulaya.

Pia, mkongo huo unatarajiwa kuunganisha zaidi watu bilioni 3 duniani.

Akizungumza katika uzinduzi wa mkongo huo leo Agosti 10, 2023 jijini Dar es Salaam, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema uwekezaji huo ni mkubwa na utawezesha huduma kuimarika na kutoa utapunguza gharama na kwa watumiaji wa intaneti nchini.

“Nchi nzima walipowekwa machinga tutaweka ‘Free Wifi’ kwa Dar es Salaam tutaweka maeneo yote ya wazi, ikiwemo Mlimani City, lakini nawahakikisha kwenye mabasi ya mwendo kasi kutakua na ‘Free Wifi’ mabasi yote.”Amesema.

Aidha, amesema Mkongo umejengwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa na hivyo una sifa ya kuwa na kasi kubwa sana haijawai kutokea.

“Kwa sasa mikongo yote tuliyonayo nchini ina wastani wa kasi ya 16 telabite per second, mkongo wa 2 Afrika una kasi ya 180 telebite per second mara 11.25 zaidi ya kile tulichonacho.

“Hili ni jambo kubwa kwa mustakabali wa nchi yetu, utaongeza kasi ya internet zaidi ya mara 10 ya sasa, ubora wa internet nchini utaongezeka sana, utasaidia kushusha gharma za mawasiliano nchini.”Amesema.

Amesema pia utasaidia kuvuta wawekezaji nchini kama google, meta, Netflix, itatoa ajira kwa vijana na itakuza uchumi wa nchi.

“Mkongo huu ni game change kwa mabadiliko ya viwanda nchini, tehama ni njia ya mapinduzi kwenye sekta zote, kilimo, afya, utalii, elimu, madini, utawala bora na kila mahali.”Amesema

Nape amesema mkongo huo umejengwa kwa ubia kati ya Meta, China Mobile a wengineo na kwamba kituo cha kutolea huduma kinaendeshwa na airtel ambayo serikali ina ubia nao.

Amesema pia, uwepo wa mkongo huo nchi jirani zinazopakana na Bahari zitakuja kuwekeza kwenye mkongo huo na kuongeza mapato.

Habari Zifananazo

Back to top button