Ni vita wenyeji wa Jiji la Milan

Ni vita wenyeji wa Jiji la Milan

WABABE wa Jiji la Milan nchini Italia, wanatarajiwa kutupa karata yao ya kwanza Ligi ya Mabingwa barani Ulaya (UEFA) hii leo, ambapo Inter Milan watawakaribisha AC Milan saa 4:00 usiku katika Uwanja wa San Siro

Inter Milan inaingia dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kufanya vyema hatua ya robo fainali kwa kuwavurumisha Benfica kutoka Ureno kwa jumla ya mabao 5-3 kwa mechi ya mikondo miwili, ilhali AC Milan imefuzu hatua ya nusu fainali kwa kuwafunga Napoli ya Italia kwa matokeo ya jumla 2-1 katika mechi za mikondo ya nyumbani na ugenini.

Mtifuano wa hii leo unatazamiwa kuwa muendelezo wa mvutano wao unaendelea katika ligi yao ya ndani Serie A,  ambapo Inter Milan imeshashuka dimbani mara 34 na kukusanya jumla ya alama 63 hivyo kushika nafasi ya nne ya msimamo wa Ligi Kuu nchini humo.

Advertisement

Na AC Milan imefungana michezo sawa na wapinzani wao Inter Milan, ikiwa wapo nafasi ya tano ya msimamo kwa kujinyakulia jumla ya alama 61, huku Napoli ikiwa tayari imeshatwaa ubingwa Serie A kwa jumla ya alama 83 katika michezo 34 ikiwa ni mara ya kwanza baada ya miaka 30 kupita.

Mshindi wa jumla katika mchezo huo anatazamiwa kukutana na mshindi kati ya Real Madrid Hispania au Manchester City ya England, ambapo usiku wa jana walitoshana nguvu kwa kutoka sare ya bao 1-1 Uwanja wa Santiago Bernabeu.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *