Ni vita ya Mayele, Saido

MABAO matano ya kiungo mshambuliaji wa Simba Saido Ntibazonkiza aliyoyafunga Juni 6, 2023,  dhidi ya Polisi Tanzania katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara, yamechochea mbio za kuwania tuzo za ufungaji bora, akiwa nyuma ya bao moja kwa kinara Fiston Mayele.

Mayele na Saido kwa pamoja wamekuwa na msimu bora hadi sasa ligi ikielekea ukingoni, mbali na mbio za ufungaji bora lakini kwa pamoja pia wanawania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ilhali Saido, anawania pia tuzo ya kiungo bora wa ligi hiyo msimu huu, ambapo hadi kufikia mzunguko wa 29  ikiwa kila timu imesaliwa na mchezo mmoja tu, hizi hapa takwimu za nyota hao.

    MAYELE

Mayele

Michezo: 25

Mabao: 16

Nafasi za mabao alizotengeneza: 3

Hat trick: 1

Jumla amehusika kwenye mabao 19

   SAIDO

Michezo: 22

Mabao: 15

Nafasi za mabao alizotengeneza: 12

Hat trick: 2

Jumla amehusika kwenye mabao 27

Itakumbukwa, Saido amechezea klabu mbili tofauti msimu huu, ambapo alianzia na Geita Gold kisha dirisha dogo kuvuna kandarasi ya wababe wa mitaa ya msimbazi, Simba.

Kwa upande wa Mayele ubabe wake hauishii tu ndani ya mipaka ya Tanzania, lakini amekuwa bora pia katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuibuka kinara wa ufungaji, akiwa na kumbukumbu ya kupachika mabao saba.

Habari Zifananazo

Back to top button