KAMISHNA wa Jeshi la Polisi, Zanzibar Hamad Khamis Hamad amesema kughushi nyaraka za miradi mbalimbali katika taasisi za serikali na binafsi hakujapewa kipaumbele katika mapambano dhidi ya ubadhirifu na uhujumu uchumi.
Kamishna Hamad amesema hayo katika ufunguzi wa kongamano la sita la chama cha wataalamu wa udhibiti wa ufisadi ,rushwa na ubadhirifu unaofanyika kwa siku tano jijini Arusha na kuhudhuriwa na mamlaka mbalimbali za udhibiti rushwa.
CP Hamad amesema wizi kwa kughushi nyaraka kunapaswa kuangaliwa kwa jicho la kipekee badala ya kukamata mhalifu moja moja wa kawaida ni wakati sasa kutumia ripoti ya mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali (CAG) ili kuwafikisha wahusika kwenye vyombo vya sheria.
“Ni wakati sasa kwa wataalamu wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar ZAECA,Takukuru wakaguzi wa ndani serikali kwa kushirikiana na vyombo vya habari kuchambua taarifa ya CAG ili kubaini ubadhirifu unaotokea hasa katika kughushi maandishi unaopelekea serikali hasara katika usimamizi wa miradi ya serikali na taasisi za umma na binafsi”
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella kwa niaba ya Waziri wa Nchi O fisi ya Rais ,Katiba,Sheria ,Utumishi na Utawala Bora Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Haroun Ali Suleiman alitoa rai Taasisi ya Wataalam wa Udhibiti wa Udanganyifu na Rushwa na Ubadhirifu(ACFE) kushirikiana na sektetarieti za mikoa na wilaya ili kudhibiti mianya ya rushwa katika miradi mbalimbali inatotekelezwa na serikali.