NIC Bima kiganjani

KATIKA kuwaboresha huduma  zao sambamba na kuendana na maendeleo ya teknolojia, Shirika la Bima la Taifa   (NIC)  limetangaza kuja na ‘Bima Kiganjani’ ikiwa na lengo la kuhakikisha wanarahisisha huduma kwa mteja na kumfikia kwa wakati.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NIC Karim Meshack katika maonesho ya kimataifa ya biashara Sabasaba, Dar es Salaam

Advertisement

“Tuna NIC kiganjani ambayo ni ‘App’ ambayo mtu anaipakua kutoka play store na itampa maelekezo yote namna ya kujisajili, ipo kwa lugha zote mbili Kiswahili na Kingereza.”Amesema Karim na kuongeza

“ Kupitia NIC kiganjani mteja ataweza kupata huduma zote muhimu na vifurushi vyote vya bima ambavyo anahitaji na kujisajili.

Amesema, NIC kiganjani inamfikia mtanzania yeyote hata ambao wapo nje ya Tanzania na huduma hiyo mtu ataipata hata akiwa chumbani amelala akihitaji kufuatilia madai.