NIC kulipa mfao saa 24

SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) limesema kwa kuwajali wateja wake wamedhamiria kuwa kinara wa ulipaji wa fidia kwa muda mchache wa saa 24 pekee ikilinganishwa na malipo wanayojivunia sasa ya siku saba pekee

Kauli hiyo imetolewa leo Juni 29, 2023 na Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NIC Karim Meshack katika ofisi zao zilizopo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba ikiwa ni awamu ya 47

“NIC ni kampuni ya bima yenye ubora inaongoza kwa mtaji na faida, mfano takwimu za mwaka jana (2022) NIC tumeweza kupata faida ya bilioni 63 hakuna kampuni yoyote ya bima ambayo imeweza kufikia faida ya kiasi hicho.”

Aidha, amewataka watanzania kuhudhuria kwenye banda la NIC kupata elimu ya bima na kueleza kuwa wamekuja na bidhaa ambazo ni bima za Maisha, majengo, mali na ajali na bima nyinginezo ili kuwarahisishia watanzania katika kukata bima na kuwekeza katika maisha huku akisisitiza suala la kushughulikia majanga ni lao.

“Wafanyabishara wafanye shughuli za uchumi wakumbuke kuweka bima, mfano maduka yanapoungua kama hujakatia bima ndio unakuta watu wanadondoka kwa presha na wengine kupata ugonjwa wa kupooza.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x