NIC: Tumieni ‘boom’ kukata bima

WANAFUNZI wa Vyuo Vikuu wameshauriwa kutumia fedha za kujikimu maarufu ‘Boom’ kujiwekea akiba kwa kukata bima ya Beam Life ambayo itawawezesha kujiwekea  akiba kidogo kidogo

Afisa Bima wa NIC Insurance Upendo Shengena akizungumza na HabariLeo katika Maonyesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ‘Sabasaba’ katika Banda la NIC amesema Bima ya Beam life ni bima ya uwekezaji ambayo itamuwezesha mwanachuo kujiwekezea  kidogo kidogo kuanzia kiasi sh 5,000 na kuendelea kwa muda wa miaka mitano mpaka miaka 15.

“Bima hii ni nzuri, kama kuna mwanachuo ana malengo yake anaweza kukata fedha anayopewa ya ‘boom’ au ‘pocket money yake’ anaweza kujibana akaweka malengo kwa kukata bima hii, hata baada ya kumaliza chuo inaweza kumsaidia mbele ya safari kutimiza malengo yake.”Amesema Upendo

Akifafanua zaidi anasema katika bima hiyo mteja anapatiwa  faida ya uwekezaji pamoja na asilimia saba ya michango ya kila mwaka, mkataba ukifika mwisho anapatiwa  mteja kiasi alichochangia pamoja na zile asilimia saba ambazo zimejibeba  mpaka mwisho wa mkataba.

Amesema pia, wanatoa mkono  wa pole ambao unaitwa ‘Funeral benefit’ ambayo ni asilima tano ya kile kima cha bima iwapo mwenye bima akifariki au kufiwa na wategemezi wake akiwemo mwenza wake au mtoto.

“Kwa sasa tupo sabasaba tumewasogezea huduma wateja wetu. Jiwekee bima kwa manufaa ya kesho yako kwa sababu beam life unaiandaa kesho yako kuanzia leo kutimiza malengo yako ya muda mrefu au mfupi.”Amesema

 

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button