NIC yainadi bima ya safari

ILI kuwalinda wananchi wanaosafiri nje ya nchi na  majanga ya dharura, NIC Insurance, imetambulisha bima ya Safari ambayo mteja anayesafiri nje ya nchi ataweza kunufaika

Hii ni bima inayokulinda dhidi majanga ya kiuchumi, upotevu au uharibifu unaoweza kutokea ukiwa umesafiri nje ya nchi.

Akizungumza na HabariLeo  Afisa Bima  wa NIC, Hopegeorge Nganisa amesema bima hiyo inaweza kukupa fidia ya  kucheleweshwa kwa vifurushi au mzigo wako,msaada wa kisheria kwa matukio kama kughairishwa au kufutwa  kwa safari katika dakika za mwisho na matibabu  ya dharura safarini, iwapo utafariki ukiwa safarini na iwapo umevamiwa na kupoteza fedha na nyaraka

Advertisement

“Unaweza kuchukua bima ya safari fupi kuanzia siku tano hadi saba, unaweza kuchukua ya mwezi mmoja au safari ndefu za kimataifa  kwa miezi sita, mwaka inategemea na safari yako.”Amesema Nganisa na kuongeza

“Bima hii ni ya hiyari ingawa kuna baadhi ya nchi ni lazima uwe na bima hii ili kuweza kwenda kwenye inchi hizo.”Amesema

Aidha Nganisa ameshauri kuwa ni vyema mtu anaposafiri nje ya nchi kupata bima hiyo bila kujali ni kwa hiyari au ni kwa mujibu wa sheria ya nchi anayokwenda.

Amesema, bima hiyo ni gharama nafuu na itakupa amani ya moyo ukiwa safarini .

 

1 comments

Comments are closed.

/* */