NIDA yakabidhi vitambulisho 16,400 Kitaya, Nanyamba

NIDA yakabidhi vitambulisho 16,400, Kitaya, Nanyamba

MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa nchini (NIDA), imetoa vitambulisho 16,400 kwa wakazi wa Kata ya Kitaya, Kiromba, Namtumbuka pamoja na Nanyamba wilayani Mtwara, mkoani Mtwara

Ugawaji huo umefanywa na maofisa wa mamlaka hiyo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya katika Kata ya Kitaya leo Disemba 19, 2022.

Mkuu huyo aliongozana na Mwenyekiti wa CCM, Mtwara Vijijijini Nashir Pontiya, Katibu Clement Bakuli na iongozi wa Halmashauri ya Mji wa Nanyamba wakiongozwa na Jamal Kapende na Mkurugenzi Thomas Mwailafu.

Advertisement

Kyobya amewasisitiza wananchi kutunza vitambulisho hivyo na kwamba wananchi wote wa kata za mpakani watapata vitambulisho vyao.

Ameongeza kuwa, Kata ya Kitaya imeletewa Sh milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya na Sh milion 100 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matano.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *