Nigeria yakamata lori 21 za chakula zikienda nje

NIGERIA imekamata malori 21 yakiwa na chakula kuelekea Chad, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Cameroon huku kukiwa na uhaba wa vyakula nchini humo

Uhaba huo unahusishwa na magendo na umezua maandamano katika majimbo kadhaa.

Tume ya Uhalifu wa Kiuchumi na Kifedha (EFCC) ilifichua chakula kilichofichwa Kaskazini-Mashariki mwa jimbo la Borno.

“Kukamatwa kwa lori hizo kunatarajiwa kukomesha wimbi la uhaba wa chakula unaosababishwa na tabia mbaya za wasafirishaji nchini kote,” EFCC ilisema.

Serikali ya Nigeria inapanga kuanza kusambaza tani 42,000 za nafaka kote nchini ili kuzima hasira ya umma kutokana na kupanda kwa bei ya vyakula.

Mgogoro wa chakula nchini Nigeria kwa kiasi fulani umelaumiwa kutokana na uamuzi wa Rais Bola Tinubu kusitisha ruzuku ya mafuta mwezi Mei mwaka jana.

Habari Zifananazo

Back to top button