Nikki: Muziki bado pasua kichwa

MSANII wa HipHop, Nicas Mchuche’Nikki Mbishi ‘amesema haamini kwenye mauzo ya muziki yanayofanyika kupitia majukwaa ya mitandao.

Mwanamuziki huyo amesema hiyo ndio sababu  ya kuamua kusambaza  albamu yake  mpya ya katiba yeye mwenyewe.

Nikki anasema hafikirii kama Tanzania imesonga mbele kwenye suala la mauzo ya muziki mitandaoni kwani malipo yake yamekuwa hayatoi taswira njema akilinganisha  na wakati ambao hakukuwa na mauzo ya mitandaoni.

“Huwezi kusema sasa hivi muziki unakuwa au unaenda mbele wakati zamani mtu hajamaliza kazi ashapewa fedha, lakini sikuhizi  unamaliza kazi, unatoa albamu unaitangaza alafu unakuja kupewa milioni moja baada ya miezi minane” amesema Nikki

Nikki Mbishi anaendelea kuisambaza albamu yake mpya ya katiba aliyoiachia wiki nne zilizopita na ameamua kuiuza kupitia mitandao binafsi.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button