“Nimefurahishwa wananchi kuchangia ujenzi wa zahanati”

WANANCHI wameshauriwa kujijengea utamaduni wa kushiriki na kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo na kuacha tabia ya kuitegemea serikali pekee.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bagamoyo, Abdusharifu Zahoro aliyasema hayo jana wakati wa zoezi la mbio za bendera za chama hicho katika kata ya Zinga, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Amesema wananchi wanapaswa kujijengea utamaduni wa kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo hatua ambayo itaisaidia kutatua changamoto zao haraka badala ya kuisubiria serikali.

“Nimefurahishwa na hatua ya wananchi wa kata hii ya Zinga kuchangia ujenzi wa zahanati yao niwapongeze sana na nimefurahishwa wao wamechangia milioni 15 sio pesa kidogo, serikali lazima tuisaidie na tuibue miradi ya maendeleo.

” alisema.

Aidha amesema serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi za maendeleo kwa Wananchi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi na kwamba hatua hiyo ni muhimu Kwa ushindi wa chama hicho.

“Mbio hizi za bedera zimeibua mambo mengi na tumejionea mengi lakinI kubwa serikali chini ya kiongozi wetu Rais wa Tanzania Samia Suluhu tunampongeza kw jitihada zake za hali na mali katika kuwasaidia Wananchi katika miradi ya maendeleo.”alisema

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Chama Cha mapinduzi, Abubakari Mlawa aliitaka jamii kujijengea utamaduni wa kuibua vitendo vya matukio ya kikatili vinavyoendelea kutokea katika maeneo yao.

“Vitendo vya ukatili wa kijinsi katika maeneo yetu ni vingi naombeni muwe mnatoa ushirikiano katika vyombo vinavyoshughulikia mambo haya ili kuweza kuthibiti masuala hayo yasiendelee kwa maslahi yetu na ya vizazi vijavyo”alisema

Diwani wa kata hiyo, Mohamed Mwinyijuma ameema wananchi wamechangia zaidi ya Sh milioni 15 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kata hiyo ili kuendelea kupata huduma za matibabu baada ya jengo la awali kujaa maji msimu wa mvua.

Alisema wananchi zaidi ya 18,000 wa kata hiyo, wamekuwa wakikosa huduma bora za matibabu katika msimu wa mvua kutokana na zahanati hiyo kujaa maji na huduma kuhamishiwa katika jengo la serikali ya mtaa.

“Kipindi cha msimu wa mvua, huduma za matibabu katika zahanati yetu tunashindwa kupata maana zahanati Ile inajaa maji na maji hukauka baada ya miezi mitatu”alisema

Habari Zifananazo

Back to top button