Nishati isiyochafua mazingira kuipaisha Tanzania

DSM; TANZANIA imetajwa kuwa na nafasi kubwa ya kuwa mzalishaji wa wa nishati safi isiyochafua mazingira kupitia madini ya graphite, colbat, manganese na nikeli
Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini Anthony Mavunde jijini Dar es Salaam katika kikao cha wadau wa madini zikiwemo taasisi za umma na binafsi zinazojishughulisha na Sekta ya Fedha chini ya Mwamvuli wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA).
Amesema, ifikapo mwaka 2050 mahitaji ya madini hayo duniani yatafikia tani milioni 150.
Kufuatia hali hiyo, amesema sekta ya madini ni sekta ambayo endapo itafungamanishwa na sekta nyingine itawezesha watu kupata mafanikio, tija, uwekezaji na maendeleo.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dk Venance Mwasse, wakati akitoa wasilisho amesema uchimbaji mdogo ni eneo ambalo linapaswa kuangaliwa kwa jicho la pekee na taasisi za fedha.
Mwasse amesema serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi kisheria katika shughuli za uchimbaji mdogo ikiwemo kuliwezesha Shirikisho la Vyama Vya Wachimbaji Tanzania (FEMATA) kuwa na uwakilishi Tume ya Madini, kuwatengea maeneo na kuwapatia elimu.
Amesema, changamoto za ukosefu wa masoko, teknolojia duni, kutokukopesheka, elimu, na kueleza kuwa, tayari STAMICO imechukua hatua kadhaa ikiwemo kuandaa mpango kutoa elimu kwa kuzunguka nchi nzima, kusaini makubaliano na GST kuwezesha kupatikana kwa taarifa za kijiolojia, kusaini hati za makubaliano na baadhi za benki.
Mwasse amesema yote hayo yamefanyika ili kupunguza hatari kwa taasisi za fedha na hivyo kuzitaka taasisi hizo kujenga imani na wachimbaji kwa kuwa tayari serikali imeingilia kati ikiwemo kuwarasimisha.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TBA, Theobas Sabi ameishukuru wizara kwa mkutano huo ambao umeziwezesha tasisi za fedha kuielewa sekta ya madini.
Amesema kutokuwepo kwa taarifa za kujua kiasi cha madini kilicho kwenye leseni za wachimbaji ni eneo ambalo limekuwa changamoto kwa mabenki na kueleza kuwa, taasisi hizo zitayachukua yaliyozungumzwa katika mkutano huo kwa ajili ya kuyajadili kwenye vikao kazi vya jumuiya hiyo.

Habari Zifananazo

9 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button