NIT watakiwa kutoa mafunzo kupunguza gharama za usafirishaji

CHUO cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimeagizwa kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa madereva, maofisa usafirishaji ili kupunguza gharama za usafirishaji serikalini na ajali zinazoweza kutokea barabarani.

Akizungumza leo mkoani Mtwara wakati akifungua mafunzo ya siku tano yanayoendelea mkoani humo kwa madereva na maofisa hao, Mkuu huyo wa Mkoa  Kanali Ahmed Abbas amesema elimu hiyo ikawe chachu ya kupunguza ajali zisizokuwa za lazima, uharibufu wa magari ili kuipunguzia serikali gharama.

Washiriki hao 56 wasisitizwa kuishukuru serikali kwasababu kuaminika kwa serikali hiyo kumesababisha mafunzo hayo kufanyika.

Mafunzo hayo yamefunguli leo Novemba 20, 2023 yanayoendeshwa na chuo hicho na kufadhiliwa na Benki ya Dunia.

Mafunzo hayo yanafanyika katika kanda ya Kusini ikiwemo mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma yatayoendelea kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Lengo likiwa ni pamoja na kuzidi kuwajengea uwelewa washiriki hao ili kuipunguzia serikali gharama hizo za uendeshaji.

‘’Niwaaombe washiriki wa mafunzo, waione ni heshima kubwa ambayo taifa imepewa pia wakione chuo hicho kuwa kimepewa heshima kubwa kuwapatia mafunzo wataalam hao.

“Vitu vyote mlivyovipata kwenye mafunzo mviweke kwenye vichwa vyenu ili muwe mstari wa mbele kupambana na kuzuia changamoto zote zilizozisema ikiwemo ajali, uharibifu wa vyombo vyetu.

” amesema Abbas

Hata hivyo wajiendeleze kielimu ili kuendana na mabadiliko ya tekinolojia ya sasa ikiwemo gari lenyewe, mifumo ya kawaida na barabara.

Aidha kwa sasa wana barabara zaidi ya moja hivyo wasipokuwa makini na mabadiliko hayo wanaweza kuwa chanzo cha kusababisha ajali za barabarani badala ya kuzizuia.

  1. Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Dk John Mahona amesema lengo la NIT kuja mkoani humo ni kwamba serikali ina magari mengi na matumizi makubwa ya serikali hiyo yapo katika magari hivyo elimu hiyo itasaidia waweze kujifunza kutumia vizuri magari  hayo.

Hali hiyo itasaidia serikali iweze kupunguza matumizi yake, kuendeleza tekinolojia hiyo iliyopo sasa kwa uadilifu na uaminifu.

Habari Zifananazo

Back to top button