Njia hii hapa kushuhudia AFCON

MTANDAO: Shirikisho la mpira wa Miguu nchini TFF limetoa utaratibu kwa mashabiki wanaotaka kusafiri kwenda kuipa nguvu timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) katika michuano ya AFCON makala ya 34 inayotarajiwa kutimua vumbi Januari 13 nchini Ivory Coast.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirikisho hilo Januari 04, 2024 ni kuwa wanaotaka kwenda Ivory Coast wanatakiwa kuomba viza kwa njia ya mtandao kupitia mtandao wa www.snedai.ci.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa wasafiri hao wanapaswa kuwa wamepata chanjo ya homa ya manjano.

Advertisement