Njia nyeupe kuifuata Stars Ivory Coast

DAR ES SALAAM: KUELEKEA michuano ya AFCON  mwakani, ambayo Taifa Stars imefuzu, wapenzi wa soka nchini wameletewa kampeni Twenzetu Ivory-Coast Ki-VIP 2024.

Stars imefuzu fainali hizo za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Ivory Coast, ambapo itarusha karata yake ya kwanza kwa kumenyana na Morocco Januari 17, 2024 kabla ya kucheza na Zambia Januari 21 na kunyukana na  DR Congo Januari 24.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Afisa Habari wa michezo ya kubashiri nchini Betika, Rugambwa Juvenalius amesema kampeni hiyo ni kwa wateja wa Betika wanaotumia mtandao wa Tigo.

Amesema, droo kubwa ya kupata mabingwa sita watakaoshinda wataenda Ivory Coast itafanyika Januari 2, 2024 na mabingwa watapata huduma za Ki-VIP kuanzia wakiwa nchini Tanzania mpaka kufika Ivory Coast.

“Huduma watakazopata ni tiketi za ndege kwenda na kurudi, hotelini kwa siku zote ndani Ivory Coast, usafiri wa kifahari kuelekea uwanjani na pia titeki ya kutazama mechi uwanjani.

Aidha, amesema jinsi ya kushirika ni kuweka pesa katika akaunti yako ya Betika kupitia Tigo Pesa na kisha kufanya ubashiri za mechi mbalimbali kila siku na kwamba washindi watatangazwa kwenye mitandao ya kijamii ya Instagram na Facebook.

 

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button