Njia tatu umeme wa uhakika SGR

DAR ES SALAAM: MENEJA Maendeleo na Biashara wa Shirika la Umeme (TANESCO), Mhandisi Magoti Mtani amesema reli ya SGR itakua na njia (lots) tatu za kusafirishia umeme wa uhakika muda wote ili kuifanya treni hiyo itoe huduma kwa uhakika.

Mtani, ameyasema hayo leo Machi 27,2024 katika kilele cha Kurasa 365 za Mama, ikiangazia mafanikio ya miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

“Hivyo basi, umeme wake utatoka katika njia ambazo zimeunganishwa kutoka maeneo mbali mbali na hii limeweza kufanyika kwa Lots 3 na ya kwanza ni Msamvu – Ihumwa (Lot 1 ina double circuits ambapo inajumuisha Lot 1 – 2 kwa pamoja na Lot ya 3 ni kutoka Isaka – Mwanza,” amesema.

Amesema, kuna uwekezaji mkubwa unafanyika katika kufanya umeme kuwa wa uhakika nchini

“Serikali imefanya kila liwezekanalo na sisi kama shirika, tunahakikisha fedha tunazopewa zinatumika katika mazingira ambayo ni sahihi na mazuri kuhakikisha hali ya umeme nchini inakuaa nzuri, ” amesema Mtani.

Amesema, mpaka sasa miradi yote ya kimkakati ya umeme inayotekelezwa nchini imetumia jumla ya Sh trilioni 8, katika fedha hizo Sh trilioni 7.2 ni fedha za ndani kwa ufadhili wa Serikali Kuu na kutoka kwa wafadhali wa nje ni Sh trilioni 1.69.

Habari Zifananazo

Back to top button