Nkasi wakabidhiwa boti 4 za doria

RUKWA; Nkasi.Mradi shirikishi wa ulinzi wa rasilimali za uvuvi Ziwa Tanganyika unaotekelezwa na Taasisi ya TNC umekabidhi kwa serikali ya Wilaya ya Nkasi, mkoani Rukwa boti nne za doria zenye thamani ya Sh milioni 200 kwa ajili ya ulinzi wa rasilimali za uvuvi ziwani humo.
Boti hizo zimekabidhiwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Riziki Shemdoe kwa niaba ya halmashauri, lengo likiwa kudhibiti uvuvi haramu, kulinda ,mazalia ya samaki, kuongeza mazao ya uvuvi, kuongeza kipato cha wadau wa uvuvi na kuongeza mapato ya serikali.
Mkurugenzi wa mradi huo, Peter Limbu amesema kuwa sambamba na hilo pia mradi unatarajia kutumia kiasi cha Sh milioni 230 kuwapeleka mafunzo ya ulinzi na ukakamavu Pasiansi Mwanza, vijana 50 kutoka kwenye vikundi vya ulinzi shirikishi vya Rasilimali za Uvuvi Mwambao wa Ziwa (BMU), ambao ndiyo watakuwa wasimamizi wa mpango huo.
Akipokea boti hizo Prof. Shemdoe amesema kuwa serikali imedhamiria kutumia sekta ya uvuvi kama moja ya maeneo ambayo yatatoa mchango mkubwa kwenye pato la taifa, hivyo msaada huo wa TNC unatekeleza malengo ya serikali kufanikisha.
Ameishukuru TNC kwa msaada huo, huku akiitaka Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi na vikundi vya ulinzi shirikishi wa rasilimali za uvuvi ziwa Tanganyika kutumia boti hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ya kulinda rasilimali hizo na kuongeza mazao ya uvuvi yanaotoka ziwa Tanganyika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi cha BMU Mkinga, Abdallah Moshi amesema kuwa boti hizo zitakuwa na msaada mkubwa kwao katika kuzuia uvuvi haramu, kulinda mazao ya samaki na kuongeza mazao ya uvuvi kwa kiasi kikubwa.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x