Chelsea imekamilisha usajili wa Christopher Nkunku kutoka RB Leipzig kwa mkataba wa miaka sita.
Chelsea imemsajili mshambuliaji huyo kwa dau la pauni milioni 60.
“Nina furaha sana, kazi kubwa imefanyika mimi kuwepo hapa, nakwenda kuwaonesha mashabiki kile nachoweza kufanya.” Amesema Nkunku baada ya usajili huo.
Usajili huo ni wa kwanza kwa Chelsea dirisha hili , huku ikiwa haina uhakika wa kuendelea kubaki na Aubameyang na Havertz ambao wote wamekuwa wakicheza nafasi za mbele.