Nkunku nje mwezi mmoja

MSHAMBULIAJI, Christopher Nkunku ameumia tena, hivyo atakuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja.

“Tulipewa taarifa kuwa Chris Nkunku ameumia”. amesema kocha wa Chelsea, Pochettino.

Nkunku alipata jeraha katika mchezo wa fainali ya Carabao Cup dhidi ya Liverpool Jumapili iliyopita.

Advertisement

Amekuwa na historia ya majeruhi tangu akiwa RB Leipzig, kabla ya kusajiliwa kwenda Chelsea.

Kwa taarifa hiyo, Nkunku ataonekana tena uwanjani mwezi wa nne.