Nkunku yupo tayari

MENEJA wa Chelsea, Mauricio Pochettino amesema mshambuliaji Christopher Nkunku atakuwa sehemu ya kikosi kitakachomenyana na Sheffield United leo.

Nkunku alijiunga na ‘The Blues’ kwa pauni milioni 52 kutoka RB Leipzig msimu wa joto lakini alipata jeraha la goti la kushoto wakati wa mechi ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya huko Chicago.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alifanyiwa upasuaji mwezi Agosti na hajaonekana kwenye Premier League kwa klabu yake mpya.

“Ni habari njema sana kwetu na ni wakati wa kuwa watulivu na utulivu kwa sababu hatutaki kumpa shinikizo.”

Nkunku alifunga mabao 16 katika mechi 25 za Ligi ya Ujerumani Bundesliga msimu uliopita na ameichezea nchi yake mechi 10.

Alikuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Pochettino baada ya Muagentina huyo kuchukua jukumu la kuinoa Stamford Bridge mwezi Mei.

Kabla ya jeraha lake, Nkunku alikuwa alionesha kiwango kizuri katika ziara ya Chelsea ya kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani kwa kufunga mabao matatu katika mechi tano.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button