NMB yafanya kweli Bunge Bonanza

BENKI ya NMB imetoa kiasi cha Sh Mil 130 kudhamini bonanza la michezo la Bunge linalotarajiwa kufanyika kesho Jumamosi Septemba 2, 2023 mkoani Dodoma.

Akizungumza mjini Dodoma leo, Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Janeth Shango amesema kati ya fedha hizo Sh Mil 90 ni kwa ajili ya vifaa mbalimbali vya michezo kwa ajili ya bonanza hilo.

Amesema benki hiyo mara kwa mara imekuwa ikishirikiana na wabunge katika matukio tofauti ikiwemo kudhamini bonanza lao, ambapo katika bonanza la Februari mwaka huu walidhamini kwa Sh milioni 100.

Naye Mwenyekiti wa Bunge Bonanza, ambaye pia ni Mbunge wa Makete, Festo Sanga ameshukuru kwa udhamini huo na kusema kuwa michezo mbalimbali itachezwa.

Ametaja baadhi ya michezo hiyo kuwa ni mpira wa miguu, netiboli, mpira wa kikapu, wavu, kukimbiza kuku, mdako na michezo mingine mbalimbali.

Amesema bonanza hilo litahusisha wabunge pamoja na watumishi wa bunge na kueleza kuwa wana matumaini makubwa litakuwa la aina yake.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button