Noah yasombwa na maji, yaua 5 familia moja

WATU watano wa familia moja wamekufa, baada ya gari yao aina ya Noah yenye namba za usajili 499 DMY kusombwa na maji katika barabara ya Arusha-Moshi eneo la Kata Amalula, wilayani Arumeru, mkoani Arusha.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Emanuel Mtatifikolo aliwataja waliokufa na miili ya kuonekana ni Angela Metili (26), Martha Metili (40) na Colin Lyimo (16), mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ilboru Arusha.

Mtatifikolo alisema maiti mbili ambazo miili yao bado haijapatikana baada ya kupelekwa umbali mrefu na maji ni pamoja na mwili wa Brenda Amani (26) mfanyabiashara na mkazi wa Ilbolu na Lisa Metili (8) mwanafunzi wa shule ya Msingi Ilboru Arusha.

Alisema dereva wa Noah la Neiman Metili, yeye alitoka akiwa mzima baada ya kufanikiwa kuchomoka katika usukani na kutelekeza gari lililosombwa na maji yaliyokuwa na kasi kubwa.

Mkuu wa Wilaya hiyo alitoa pole kwa familia, ndugu na jamaa waliopoteza wana familia kwani msiba ni mkubwa, ambapo walikuwa wakienda katika mahafali ya kidatu cha sita mkoani Kilimanjaro.

Habari Zifananazo

Back to top button