Historia imewekwa Ligi ya Mabingwa Ulaya
KIUNGO Mtanzania, Novatus Dismas ameingia kwenye orodha ya wachezaji waliowahi kucheza mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kucheza usiku huu kati ya timu yake ya Shaktar Donetsk dhidi ya FC Porto.
–
Wachezaji wengine waliowahi kucheza mashindano hayo ni Kassim Manara akiwa na Admira ya Austria na Mbwana Samatta akiwa na Genk ya Ubelgiji.
–
Katika mchezo huo, mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika, Shaktar walikuwa nyuma kwa mabao 3-1.