Ntakarutimana achaguliwa Spika EALA

WABUNGE wa Bunge la  Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA), wamemchagua Joseph Ntakarutimana kuwa Spika wa bunge hilo katika uchaguzi uliofanyika leo mjini Arusha.

Ntakarutimana ambaye  amekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Tawala nchini Burundi cha  (CNDD-FDD).

Spika huyo amekua  ni mgombea pekee wa nafasi hiyo baada ya wagombea wawili kutoka nchini Sudani Kusini, Gai Deng na Dk Anne Itto kujitoa dakika  za mwisho na hivyo kusababisha mgombea huyo kukosa ushindani.

Akisimamia uchaguzi huo , Katibu wa Bunge la EALA, Alex Obatre alitoa  nafasi kwa wagombea hao waliojitoa kutamka kwa vinywa vyao kuwa wamejitoa, baada ya kuwasilisha taarifa rasmi ya kujitoa, ambapo walisimama na kusema wanamuunga mkono mpinzani wao.

Katika upigaji kura Spika huyo mpya alipata kura za ndiyo 54 kati ya kura 63 za wabunge  wote kutoka nchi saba wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ambapo kura nane ziliharibika na kura moja haikupigwa kabisa.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button