Ntibazonkiza bado hajapata ofa

KIUNGO mshambuliaji wa Geita Gold FC, Saido Ntibazonkiza, leo Desemba 13 amesema hajapata ofa yoyote kutoka klabu yoyote hapa Tanzania.

Akizungumza na SpotiLeo, kiungo huyo mwenye mchango mkubwa kwenye kikosi cha Geita FC, ameeleza kuwa taatifa za yeye kutakiwa na timu ya Simba amekuwa akizisikia kupitia vyombo vya habari lakini hakuna kiongozi yeyote wa timu hiyo aliyenfuata.

“Uvumi wa Mimi kutakiwa na Simba nausikia lakini ukweli sijapokea ofa yoyote kutoka timu yoyote hapa Tanzania, kwa sasa nipo Kambini na timu yangu ya Geita tukijiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu,” amesema Ntibazonkiza.

Kiungo huyo amesema kwa sasa hawezi kuzungumzia chochote kuhusu Simba kumuhitaji sababu bado anamkataba na Geita na Simba kama wanamihitaji wanapaswa kuzungumza na viongozi wake siyo yeye.

Ntibazonkiza tangu ajiunge na timu hiyo katikati ya mzunguko wa kwanza ameifungia timu hiyo amekuwa kinara katika kutoa pasi za mwisho na ameshafunga mabao matatu kwenye ligi kuu.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x