NYOTA wa Simba Saido Ntibazonkiza na mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele wamefungana kwenye mbio za ufungaji bora wote wakiwa na magoli 17 kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.
Ntibazonkiza amefunga mabao mawili kwenye ushindi wa bao 3-1 wa Simba dhidi ya Coastal Union huku Mayele akifunga bao moja kwenye ushindi wa Yanga wa mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons.
Pazia la ligi kuu Tanzania bara limefungwa rasmi leo hii na Yanga wakikabidhiwa taji lao la 29 msimu huu.
Comments are closed.