Nyangumi apindua mashua, mmoja afariki

MTU mmoja amekufa na mwingine amelazwa hospitalini huko Australia baada ya nyangumi kugonga na kupindua mashua yao ndogo wakati wakifanya shughuli za uvuvi, mamlaka imeeleza.
–
Wanaume hao wawili walirushwa kutoka kwenye mashua hiyo ilipogongwa majira ya saa 12 alfajiri ya leo karibu na La Perouse, kilomita 14 Kusini Mashariki mwa Sydney.
–
Watu waliokuwa kwenye mashua ya pili walipaza sauti baada ya kuona meli ya mita 4.8 ikiwa haina mtu ndani ya maji, polisi walisema.
–
Mwendesha mashua mwenye umri wa miaka 53 aliokolewa na kutibiwa na wahudumu wa afya na kupelekwa hospitalini, ambapo alikuwa katika hali nzuri, kulingana na mamlaka.
–
Mwanamume wa pili, mwenye umri wa miaka 61, alifariki katika eneo la tukio.
–
Boti hiyo “inawezekana iligonga au kuathiriwa na uvunjifu wa nyangumi, na kusababisha mashua kupinduka, na kuwarusha watu wote wawili”, polisi walisema katika taarifa.



