MWANAMUZIKI kutoka Kenya, Nyamari Ongegu ‘Nyashinski’ amewasili leo Oktoba 20, 2023 Dar es salaam kutubuiza katika tamasha kubwa la “Serengeti Lite Oktoba Festival” litakalo fanyika kesho Oktoba 21, 2023 katika fukwe ya Coco Dar es salaam.
Nyashinski amesema kajipanga vizuri kutoa burudani ya kutosha kwa mashabiki watakao hudhuria tamasha hilo.
Ameongezea kua ni bahati ya kipekee kupanda jukwaa moja na wasani wenye majina wakubwa watakao tumbuiza hiyo kesho.
Tamasha hilo litakutanisha wasani wakubwa kutoka Afrika Mashariki, kwa Tanzania atakuwepo Ali Kiba Billinas, Chino kidd, Gnako pamoja na wengine wengi, na kutoka Uganda atakuwepo Joseph Mayanja anaejulikana kwa jina la Jose Chameleone.