MLINDA lango wa Yanga Djigui Diarra amewapa matumaini mapya mashabiki wa timu hiyo kuelekea mchezo wa mkondo wa pili fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya USM Alger utakaopigwa nchini Algeria Juni 3.
Kupitia mtandao wake wa Instagram Diarra ameandika bado anaamini wanaweza kuandika historia
” Mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho unachezwa kwa dakika 180, tumepoteza mchezo ila hatujashindwa vita, tutarudi tukiwa imara zaidi na kwa pamoja tutaandika historia” aliandika Diarra
Yanga wanakwenda kwenye mchezo huo wa ugenini wakiwa na rekodi ya kushinda michezo mitatu ugenini tangu hatua ya makundi hadi sasa huku wakipata sare mchezo mmoja na kupoteza mchezo mmoja.
Comments are closed.