Nyie Yanga mtaua watu jamani!

NYIE Yanga mtaua watu jamani kwa hizi raha! Pengine ndivyo unavyoweza kuzungumzia ushindi wa mabao 2-0, ambao Yanga imeupata baada ya kuifunga Marumo Gallants ya Afrika Kusini.

Mchezo huo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika umemalizika jioni hii Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, hivyo kwa matokeo hayo ili Yanga ifuzu fainali inahitaji sare ya aina yoyote au isifungwe zaidi ya bao 1-0 kama ikishindwa kushinda mchezo wa marudiano nchini Afrika Kusini wiki ijayo.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Stephane Aziz Ki dakika ya 64 na Bernard Morrison dakika 90+2.

Advertisement

 

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *