WACHEZAJI kutoka Ulaya sasa watapata nafasi ya kuitumikia klabu ya Simba, hivyo hivyo kutoka Simba watapata nafasi ya kwenda kukipiga Ulaya. SpotiLeo imeelezwa.
Hatua hiyo imekuja baada ya leo Juni 7, 2023 Simba SC kusaini mkataba wa ushirikiano na timu ya West Armenia kutoka nchini Armenia, mkabata utakaotoa nafasi kwa klabu zote mbili kuuziana wachezaji.
“Leo tumeingia mkataba wa ushirikiano na timu ya West Armenia Football Club. Mkataba huu wa ushirikiano unatoa fursa kwa kuuziana wachezaji, maendeleo ya ufundi, soka la vijana na maendeleo ya soka.” Imeeleza taarifa ya Simba SC.
West Armenia ni timu inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Armenia, timu hiyo ndio bingwa wa sasa wa ligi hiyo.