Nyota wa Yanga afiwa na mtoto

KIUNGO wa Yanga, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, amefiwa na mtoto wake aitwaye Feisal Salum katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam, Yanga SC imeeleza.

Taarifa iliyotolewa na kitengo cha habari na mawasiliano leo Machi 7, 2023 imeeleza kuwa Yanga inatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huo.

“Klabu ya Yanga tunatoa pole kwa mchezaji wetu Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kwa kufiwa na mtoto wake Feisal Salum kilichotokea asubuhi leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,” imesema taarifa hiyo.

Salum Abubakar ni mtoto wa gwiji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Abubakar Salum ‘Sure Boy’.

Habari Zifananazo

Back to top button