Nyota wa zamani Brazil afariki dunia

MARIO Zagallo, bingwa mara nne wa Kombe la Dunia akiwa mchezaji na kocha wa Brazil, amefariki akiwa na umri wa miaka 92.

Zagallo alishinda Kombe la Dunia mfululizo mnamo 1958 na 1962 kabla ya kusimamia ubingwa wa nchi yake mnamo 1970 akiwa meneja na kisha kama kocha msaidizi mnamo 1994.

Zagallo, ambaye pia aliipeleka Brazil fainali mwaka 1998 ambapo walifungwa na Ufaransa, amekuwa mtu wa kwanza kushinda Kombe la Dunia akiwa mchezaji na meneja.

Ujumbe wa mtandao wa kijamii uliotumwa kwa akaunti ya Instagram ya Zagallo ulisomeka: “Ni kwa masikitiko makubwa kwamba tunatangaza kuaga dunia kwa bingwa wetu wa milele, Mario Jorge Lobo Zagallo.

Habari Zifananazo

Back to top button