Nyumba za waathirika wa tope kukamilika Disemba

NYUMBA 47 zinazojengwa na Kampuni ya Diamond Williamson Ltd inayochimba madini ya Almas eneo la Mwadui wilayani Kishapu mkoani Shinyanga kwa waathirika wa tope wanatarajia kuzikamilisha mwezi Disemba mwaka huu.

Hayo yamesemwa tarehe 13,Novemba,2023 na mwakilishi wa meneja wa kampuni hiyo mhandisi Shagembe Mipawa alipokuwa akiwasilisha taarifa ya ukamilishaji wa ulipaji wa fidia na walivyofanya uchunguzi kwa kila kaya ilivyoathirika mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa.

Mhandisi Shagembe amesema bwawa hilo linatarajia kutunza ujazo wa maji tope tani million 2.6 na kudumu katika miaka miwili ijayo ambapo wamekuwa wakilikagua wao na maafisa mazingira kutoka nje ya mgodi huo kuhakikisha liko salama halileti tena athari kwa wananchi.

“Tumepata changamoto kubwa kwani uzalishaji ulisimama zaidi ya mwaka mmoja na mwezi Agosti mwaka huu tumekutana na tatizo la nishati ya umeme kukatika kwani tumekuwa tukitafuta njia mbadala ya kupata nishati hiyo.”Mhandis Shagembe.

Mhandisi Shagembe alisema wameuza dola 250 kwa mauzo ya kwanza na sasa wanasubiri mauzo ya pili kwani kufikia mwezi Oktoba mwaka huu wamezalisha tani zaidi ya milioni 1.4 na karati 106,000

Meneja mahusiano wa kampuni hiyo Bernad Mihayo amesema walitenga Sh bilioni 1.8 kwaajili ya ujenzi wa nyumba 47 zilizoathiriwa na tope lililokuwa linatiririka kwenda kwenye makazi hayo lakini waathirika wanne wamekataa kujengewa nyumba wanataka fedha.

Mihayo amesema kulikuwa na waathirika 304 na mmoja hafahamiki alipo na katika zoezi la ufuatiliaji kwa kina juu ya waathirika wakabaini wengine kudanganyana kueleza mali zaidi tofauti na uhalisia.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude ambaye alikuwa mwenyekiti wa kamati iliyoundwa na mkuu wa mkoa amesema watu wote wapokee fidia kwa mujibu wa sheria maeneo yao yamethaminishwa kama ilivyokuwa wameneo yao ya awali na kila mmoja kupata haki yake kwa usawa.

“ Mgodi huu una hisa na serikali na kuingiza mapato mengi Ninawaomba watu wanne waliokataa kujengewa wakitaka fidia ya fedha wakubali kujengewa kwani utaratibu wa kutoa fedha haupo” amesema Mkude.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x