Nyumba za utamaduni wa Zanzibar kujengwa Kijiji cha Makumbusho

DAR ES SALAAM: MWENYEKITI wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar inayosimamia Utalii, Biashara na Kilimo, Mtumwa Pea Yusuph amesema wanatarajia kujenga nyumba za Utamaduni wa Zanzibar katika eneo maalum lililotengwa ndani ya Kijiji cha Makumbusho, Dar es Salaam kwa lengo la kuendeleza urithi wa asili na utamaduni wa makabila mbalimbali ya Tanzania.

Pea ametoa kauli hiyo wakati Wajumbe wa Baraza hilo walipotembelea Kijiji Cha Makumbusho  leo Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza na kujionea nyumba za asili za makabila mbalimbali ya Tanzania na kupata uzoefu wa namna ya kuongeza idadi ya watalii kupitia sekta ya Makumbusho na Malikale.

“Niseme tu kwamba sisi tumefarijika sana kwa ziara hii, lakini niseme kwamba tunalichukua hili na kulipeleka kwa wenzetu kuona namna gani ya lile eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya Zanzibar basi na sisi kuja kujenga kuwekeza katika eneo lile halafu baadaye na sisi kushiriki kwenye matamasha.” Amebainisha Pea.

Habari Zifananazo

Back to top button