Odinga aendelea kufuatilia kesi yake

Picha ikimuonesha mgombea Urais wa Azimio Raila Odinga akifuatilia moja kwa moja kesi aliyofungua katika Mahakama ya Juu nchini Kenya kupinga matokeo ya Uchaguzi wa Agosti 9  imezua hisia miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Picha hiyo ambayo Raila alichapisha kwenye akaunti yake ya Twitter inamuonesha akiwa ameketi juu ya kochi nyumbani kwake. Waziri Mkuu huyo wa zamani alilikiwa akitazama matukio kwenye televisheni kubwa iliyowekwa ukutani.

 

Habari Zifananazo

Back to top button