MGOMBEA urais wa Kenya kwa tiketi ya Muungano wa Azimio, Raila Odinga amesema anaheshimu uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Kenya kuhusu kesi yake ya kupinga ushindi wa Rais Mteule, William Ruto, lakini hakubaliani na uamuzi huo.
Taarifa kwa umma iliyotolewa na Odinga, muda mfupi baada ya Mahakama ya Juu ya Kenya, kutoa uamuzi kuhusu kesi hiyo leo, imesema uamuzi huo wa mahakama sio mwisho wa harakati za kutetea haki zao na daima wataendelea kutetea utawala wa sheria na katiba.