Ofisa mipango adaiwa kubaka mtoto kwenye gari

OFISA Mipango Miji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, Dickson Mwenda (37) amepandishwa kizimbani akidaiwa kumbaka mtoto wa miaka 15 ndani ya gari.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Ali Makame amesema kijana huyo alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Mlele kujibu tuhuma zinazomkabili.

Kamanda Makame aliwaeleza waandishi wa habari kuwa Mwenda anadaiwa kumbaka mtoto huyo Agosti 13 mwaka huu, saa moja na nusu usiku katika Kijiji cha Kibaoni, Kata ya Kibaoni kwenye Tarafa ya Mpimbwe wilayani Mlele.

Advertisement

Alisema mama mzazi wa mtoto huyo alikuwa na mtuhumiwa baa wakipata vinywaji, baada ya muda mama huyo alimkabidhi mtuhumiwa huyo mtoto akiwa na mdogo wake awapeleke nyumbani.

Alidaiwa kuwa wakati wakiwa njiani kwenye gari la Mwenda lenye namba za usajili T 927 DMC aina ya Toyota kijana huyo aliegesha gari pembeni ya barabara kisha akambaka mtoto huyo wakiwa kwenye gari.

Kamanda Makame alisema hadi sasa mshitakiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi.

 

 

 

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *