Ofisa Usalama feki atapeli wazazi Sh Mil 5 Katavi

JESHI la Polisi Mkoa wa Katavi, linamshikilia Geofrey Evarist (44), kwa tuhuma za kujifanya mtumishi wa serikali kutoka Idara ya Usalama wa Taifa na kujipatia fedha kwa kuwalaghai wazazi kuwa atawasaidia watoto wao kupata nafasi ya kujiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)na Usalama wa Taifa.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Ali Makame, imesema katika udanganyifu huo, mtuhumiwa alijikusanyia fedha kiasi cha Sh 5,100,000 kutoka kwa wazazi wa vijana wane.

Amesema tukio lilitokea Misunkumilo Manispaa ya Mpanda, ambapo vijana hao ambao wazazi wao wamelaghaiwa fedha wametoka mikoa mbalimbali, ambapo aliwakodia nyumba ya kuishi, ili kuendelea kujipatia fedha kutoka kwa wazazi wao.

Mtuhumiwa bado anaendelea kuhojiwa na mara baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Habari Zifananazo

Back to top button